Thursday, July 2, 2015

Anonymous

LAZIMA UKAE! Hiki Ndicho Kinachofuata Toka Kwa ALIKIBA Kimataifa Mwaka Huu!

Muimbaji wa ‘Chekecha Cheketua’, Alikiba ambaye yuko Nairobi, Kenya kwenye msimu mpya wa kipindi cha Coke Studio Africa, ametoa ahadi kwa mashabiki wake juu ya collabo ya kimataifa.

Alikiba ambaye ameachia video ya ‘Chekecha Cheketua’ wiki hii, jana alipata nafasi ya kuchati na mashabiki wake kupitia ukurasa wa Facebook wa Coca-Cola.

Miongoni mwa maswali aliyokutana nayo ni kuhusiana na collabo ya kimataifa, ambapo shabiki mmoja alimpongeza kwa kazi zake na kumuuliza ni lini waitegemee, na hili ndio jibu lake:
“Ahsante sana. Mwaka huu huu.”

Hata hivyo King Kiba hakutoa maelezo zaidi, hivyo collabo hiyo bado iko kwenye mabano. Unahisi ni msanii gani wa kimataifa ambaye Kiba anafaa kufanya naye collabo kwa kipindi hiki?

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.