Friday, July 3, 2015

Anonymous

STRAIKA wa YANGA SC, AMISSI TAMBWE Apata Ajali Ya Gari Jijini Dar

Straika wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe.
Ibrahim Mussa, Dar es Salaam
STRAIKA wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, juzi Jumatano alipata ajali baada ya gari lake aina ya Toyota Mark X kugongwa na Bajaj katika eneo la Tandale kwa Mtogole wakati akielekea mazoezini.

Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa msimu wa 2013-2014, amesema ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa Bajaj kutaka kulazimisha kupita sehemu ambayo hakutakiwa kupita kwa mujibu wa sheria za barabarani.

“Nimepata ajali leo asubuhi (juzi) wakati nakuja mazoezini pale katika eneo la Tandale kwa Mtogole, kuna Bajaj ilitokea kwa nyuma yangu, sasa dereva akalazimisha kupita katika upande wangu na njia ilikuwa ndogo, gari imeumia kwa sababu amechuna rangi na ameng’oa bampa la mbele. “Nilimsamehe palepale kwa sababu sehemu iliyoharibika haikuwa kubwa ila kama angevunja taa tungekamatana ila nitaipeleka gereji kwa ajiili ya matengenezo na ipakwe rangi ili iwe na muonekano wa awali,” alisema Tambwe.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.