Ray C anaweza kuwa amezivunja roho za wanaume zaidi ya 500
waliojipanga mstari kujibu ofa yake aliyoitangaza kwenye Instagram kuwa
anatafuta mume.
Ray C ameiambia Bongo5 kuwa mume mwema hatafutwi kwenye mitandao bali huletwa na mwenyezi Mungu.
“Huo ulikuwa utani tu,” amesema Ray C.
“Nilikuwa nataka kuwafurahisha kidogo watu wangu wa Insta. Watu wengi
sana, nimepata simu nyingi kweli kweli. Nimepokea zaidi ya simu 500
mpaka saa sita usiku. Kwahiyo nimeona mashabiki wangu bado wapo,
wananipenda sana,” amesema.
“Hapana sina mpango wa kuolewa. Mume mwema anatoka kwa Mungu, huwezi
kusema unatangaza. Mume mwema anatoka kwa Mungu nikimpata mtasikia, sasa
hivi sipo kwenye mahusiano, sina mtu yoyote.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.