Ni kipindi kirefu rapper Lord Eyez hajasikika katika kazi za wasanii wenzake wa kundi la Weusi, wala hajatoa kazi zake binafsi.
Miezi michache iliyopita Nikki wa pili alitoa wimbo wa ‘Safari’
aliowashirikisha members wa Weusi akiwemo Joh Makini na G-Nako, baadae
Joh akatoa ‘Nusu Nusu’ aliyomshirikisha G-Nako, G-Nako naye alitoa ngoma
aliyomshirikisha Joh, lakini rapper Lord Eyez hajahusika wala kutoa
ngoma zake binafsi kwa kipindi kirefu.
Msemaji wa Weusi, Nikki Wa Pili ameiambia Bongo 5 kuwa Lord Eyes bado
ni member wa kundi hilo, lakini ratiba zake binafsi zinazomfanya awe
Arusha muda mrefu ndio zimepelekea kutoshiriki kwenye kazi za members
wa Weusi ambazo mara nyingi hufanyika Dar.
“Lord Eyez yuko kwenye kundi lakini unajua sisi ni kampuni halafu inategemeana na ratiba zako binafsi.” Alisema Nikki wa Pili. “Kwa
mfano ukimwangalia Bonta yuko Kahama kwahiyo namna yake ya kurekodi
inategemeana na kazi yake, Lord Eyez kwa kipindi kirefu sana amekuwa
yuko Arusha. Kwahiyo ana kazi zake anafanya, unajuwa kila mtu anafanya
kazi zake hata mimi nafanya kazi zangu na ukiangalia huu mwaka kuanzia
umeanza mpaka saizi hatujafanya kazi ya kundi ambayo imetoka, kwahiyo
imekuwa hizi kazi za kila mtu anafanya binafsi.”
Nikki ameelezea jinsi members wa Weusi hufanya kazi zao;
“Huu ufanyaji kazi binafsi inategemea na mazingira na uko wapi,
kwa mfano kwa ‘Safari’ sio kwamba nilipanga kufanya na kina Joh, ni
kwamba walikuwepo wakati kazi inafanyika Lord Eyez hakuwepo kwahiyo
labda angekuwepo labda angeweza kuwepo. G-Nako nyimbo yake mpya ambayo
amenishirikisha nilikuwepo wakati anafanya, na unajua sisi hatuna
rules…”
“Lord Eyez saizi ni kama miezi nane hivi yuko Arusha, na sisi
kazi nyingi tumefanya huku (Dar) kwahiyo ndo maana labda amekuwa
hajaonekana sasna kwenye kazi za mmoja mmoja ambazo zimetoka lakini kazi
zake anazo. Tunasubiri yeye mwenyewe asema anataka kutoa lini kila mtu
ana ratiba yake binafsi, kwahiyo unapokuwa umejipanga then unawasilisha
kwenye kundi jamani mi kazi yangu nafanya hivi then sisi kama member
tuna support kama tunavyo sapotiana.” Alimaliza Nikki Wa Pili.

Note: Only a member of this blog may post a comment.