Wednesday, July 15, 2015

Anonymous

AY aitaja sababu ya kwanini itamchukua muda kumpenda msichana mwingine baada ya kuachana na ex wake

Ambwene Yessayah aka AY anaukaribia mwaka wa pili sasa bila kuwa na girlfriend. Ni uamuzi mgumu kwa mtu maarufu kama yeye, lakini ni nini hasa sababu ya msimamo wake huu?

“Kabla ya kuwa na yule ex wangu, nilisema huyu ndio niwe naye.. yaani kikitokea kitu kibaya yaani ya kutufanya mimi na yeye tukaachana, nilijipa hiyo nadhiri kwamba nitakaa muda mrefu sana,” AY alikiambia kipindi cha Chill na Sky cha wiki hii.

“Hata yeye anajua nilichomwambia ‘hata kama tukiachana, utakaa kwenye internet ukiangalia huyu jamaa yuko na nani utangoja sana’ kiukweli. Unaweza kukuta yeye tayari anaendelea na maisha yake, unaweza kukuta ana mtu wake maisha yanaendelea, lakini kwa upande wangu nilishajiahidi kama ikitokea wrong inabidi nijipe nafasi zaidi nione inakuaje,” aliongeza.

AY anasema sababu ya kujiwekea nadhiri hiyo ni kutokana na kumpenda sana ex wake huyo na alimuona kama mwanamke ambaye angeweza kufunga naye ndoa.

“Ilifika hiyo time kabisa ya kuweza kuwa naye pamoja na nilikuwa namuambia mara nyingi sana kwamba siombei lakini ikitokea mimi na yeye tumevurugana nitakaa pembeni muda mrefu sana.”

Hata hivyo AY anasema sababu ya kuachana kwao si kubwa kiasi hicho.

“Kupishana kwetu haikuwa sijui huyu kacheat, wala haikuwa hivyo ni kitu kingine kabisa. Sifanyi labda nimemkasirikia yeye, tunaongea vizuri na mama yake ni rafiki yangu.”
Sikiliza zaidi Chill na Sky hapo chini.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.