Matukio ya watoto wa kike kuuawa
yamekuwa yakitokea kila wakati jijini Dar es salaam.. ikiwemo tukio
lilitokea maeneo ya Kivule la mtoto kuuawa na mwili wake kukutwa ukiwa
ndani ya nyumba ambayo haijamalika na lile la mtoto kuuawa Mabibo.
Timu ya Hekaheka leo imekuja na tukio lingine lililotokea maeneo ya Tabata Msimbazi ambapo mtoto wa miaka mitano amekutwa ameuawa huku mwili wake ukikutwa na damu maeneo ya puani, mdomoni pamoja na sehemu za siri.
Mjumbe ambaye
ndiye aliyemuhudumia mtoto huyo unga baada ya kutumwa na wazazi wake
dukani alisema baada ya kumuuzia unga alionekana na mtu mmoja ambaye
alikua akiongozana naye bila kujua ni nani.
Baada ya muda wazazi wake walianza
kumuulizia bila mafanikio na kuambiwa alionekana na mtu mmoja wakiondoka
na alitafutwa bila mafanikio kisha kutoa taarifa polisi..baada ya muda
kupita walipata taarifa kuna mtoto amefariki maeneo ya Kimanga na kukutwa ni mwenyewe.
Baada ya kufanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Muhimbili alikutwa ametolewa baadhi ya vitu ndani ya mwili wake.
Isikilize hapa…

Note: Only a member of this blog may post a comment.