Thursday, July 2, 2015

Anonymous

Mwanafunzi kaona aingie na jeneza kwenye mahafali yake…

Niliwa kukuletea atori ya bibi harusi kuamua kumsuprise mume wake pamoja na wageni waalikwa siku ya harusi baada ya kuingia ukumbini akiwa ndani ya jeneza na sababu kubwa alidai anaamini anaweza kuwa amevunja rekodi ya pekee. 

Leo nakuletea hii nyingine ambayo imetokea Uingereza baada ya mwanafunzi kuamua kuingia kwenye sherehe za mahafali ya kumaliza elimu yake akiwa ndani ya jeneza wakati wenzake wakitumia magari na usafiri mwingine kwenda kwenye sherehe hiyo na hakuna aliyehisi kama angeweza kufanya kitendo hicho. 

Simom May ambaye alikuwa akisoma chuo cha Alder Grange Community and Technology School, katika mji wa Rossendale huko Uingereza,  aliingia kwenye eneo la shule akiwa ndani ya jeneza akisindikizwa na wapambe wake ambaye ni mdogo wake ambaye inasemekana ndiye alimshauri.
Kitendo hicho kilionekana kuwafurahishwa na kuwashangaza wanafunzi wenzake pamoja na walimu waliohudhuria sherehe hiyo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.