Chrissy Renny ni kijana mwenye kipaji kisicho cha kawaida – anachora
picha kwa kutumia kalamu ya wino ambayo ukiilinganisha na picha
original, unaweza kudhani aliyochora ni photocopy.
Cha kufurahisha zaidi, Chrissy ni Mtanzania na sasa jina lake limefika Marekani – thanks kwa shavu alilopewa na Ne-Yo.
Chrissy ambaye huchora picha za mastaa anaowapenda na kuziweka kwenye
akaunti yake ya Instagram, alimsurprise Ne-Yo aliyekuwa nchini Afrika
Kusini wiki iliyopita kwenye MTV MAMA, kwa kuchora picha yake.
“A pen drawing of Ne-yo can’t wait for his performance on #mtvmama
today 18 july, #nonfiction2015 #neyonation #neyo please tag him too
@neyo, aliandika Chrissy kwenye picha hiyo.
Ne-Yo ameipenda picha hiyo na hakusika kuipost kwenye akaunti yake
yenye followers milioni moja na kuandika, “This is dope! Shout out to
@chrissrenny #NEYONATION #Art #NONFICTION2015.”
Tangu aanze kuchora picha za mastaa mbalimbali, Ne-Yo ndio msanii wa
kwanza wa Marekani aliyeiweka picha hiyo kwenye akaunti yake na ndio
maana Chrissy amekipokea kitendo hicho kwa furaha kubwa.
“Am shocked thank you neyo for the appreciation and thanks to
everyone for the tags you guys are so dope @neyo @evey1,” aliandika
Chriss.
Tayari Chrissy amepata mashabiki duniani kote.
“@neyo liked and shared @chrissrenny …that’s how I came here..love
your work. Greetz from The Netherlands,” ameandika msichana mmoja kutoka
Uholanzi.
Chini ni baadhi ya picha za mastaa alizochora Chrissy.
Note: Only a member of this blog may post a comment.