NAAMINI
kila msomaji wangu yupo salama baada ya kumaliza mfungo wa Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani lakini pia baada ya sherehe za kumalizia mfungo huo
ambapo ni Sikukuu ya Idi.Mada ya wiki iliyopita ndiyo inayoendelea leo.
Kila anayekutongoza lazima umwambie mumeo?
Mada ilipokelewa kwa mitazamo tofauti sana, kila msomaji alikuwa na mawazo yake yakikinzana na wengine. Hiyo ni mitazamo tu.
Wiki iliyopita niliishia kwa kusema ukiuliza wanaume wengi kuhusu tabia hii ya wake zao kuwataja kwa wanaume zao wale wanaowatongoza, watatoa majibu tofauti kutokana na kila mmoja kuwa na mtazamo wake.Wapo wanaume hawataki kusikia, wapo wanaume wanaotaka na kuona ni sawasawa tena huwafagilia wake zao kwamba, ni waaminifu sana ndiyo maana wanakuwa wanasema kwa kila mwanaume anayemtongoza.
Lakini hata hivyo, wanaume wenye kuchekecha akili sawasawa kabla ya kutoa majibu wanatilia shaka kitendo hicho wakiamini kwamba, wanawake wenye tabia hiyo ni wale ambao kama itatokea akamkubali mwanaume huyo anayemtongoza, maana yake ni nini?
WANACHOAMINI
Baadhi ya wanaume walisema kuwa, mwanamke mwenye tabia ya kuwasema kwa mumewe wanaume wanaomtongoza ni kiashiria cha kuficha maovu.“Ukimwona mwanamke anakwambia f’lani ananitongoza, f’lani ananitaka. Maana yake ni kwamba, anataka aonekane mwaminifu ili aweze kufanya yake kwa mapana na asitiliwe shaka,” alisema Ali Kandandila, mkazi wa jijini Dar.
Mwingine
alisema mwanamke wa hivyo miaka hii na hata ya zamani hayupo. Akitokea
ana lake jambo kwa vile kitendo hicho kufanywa kwa mwanaume
anayejulikana.
“Kama mke wangu atatongozwa na fundi simu Kariakoo, atakuja kuniambia? Lazima awe mtu anayejulikana na mumewe ili kumfitinisha. Je, akitokea fundi hasa wa kutongoza akamkubalia ataniambia? Huo ni unafiki,” alisema mwanaume huyo akijitambulisha kwa jina la Baba Sai.
WANAWAKE WENYEWE
Baadhi ya wanawake wenyewe walipoongea na mimi kuhusu mada hii walionesha kutilia shaka ukweli wake.
“Kwa kweli wanawake hatutakiwi kuwa hivyo. Ila ninachojua mimi ni kwamba, mwanamke kama unatongozwa na rafiki au mwanaume ambaye mumeo anamjua, lazima uchukue hatua ya kumkanya huyo mwanaume, kwa sababu ukimsema kwa mumeo utasababisha ugomvi,” anasema dada Fenela, mkazi wa Ubungo-Maziwa, Dar.
KUNA HATUA MBILI KUFIKA KWA MUMEO
Nilibahatika kuzungumza na mzee Shauri mwenye miaka 75 sasa. Yeye anasema mwanamke anatakiwa kumwambia mumewe kuhusu mwanaume anayemtongoza, hususan kama mtu huyo atakuwa anajua huyu mwanamke ni mke wa f’lani.
“Ila kuna hatua mbili kwanza kabla ya kusema. Kwanza, mwanamke atumie kinywa chake kumwonya huyo mwanaume na kumwambia, atamsemea kwa mkewe huyo mwanaume (kama ana mke).
“Akiendelea tena, amwambie atamwambie mume wake sasa ili kila kitu kijulikane. Kama ataendelea kweli, amwambie mumewe tu ili uasi uishe,” alihitimisha mzee huyo kwa tafsiri kwamba, kama mwanamke atapitia hatua alizozitaja, bado mwanaume akaendelea kumtongoza, mambo yawekwe hadharani tu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.