Baada ya kutoa ahadi ya kuachia collabo mpya na Diamond Platnumz mwezi ujao, Davido amesema kuwa collabo yake na Wizkid pia itatoka mwezi ujao (August).
Davido ambaye jina lake halisi ni David Adeleke, weekend iliyopita alipost picha akisheherekea tuzo ya 2015 MTV MAMA Best Male akiwa pamoja na Wizkid na kuandika: “BEST MALE 2 years in a row!! DAVIDO X WIZKID DROPS NEXT MONTH!! @wizkidayo”
BEST MALE 2 years in a row!! DAVIDO X WIZKID DROPS NEXT MONTH!! @wizkidayo pic.twitter.com/oY3oES5IP8
— Davido (@iam_Davido) July 18, 2015
Licha ya collabo hizo, album mpya ya staa huyo iitwayo ‘O.B.O’
aliyowashirikisha mastaa mbalimbali akiwemo Trey Songz, Meek Mill, Akon
na wengine inatarajiwa kutoka August 10.
Note: Only a member of this blog may post a comment.