Shani Ramadhani na Mayasa Mariwata
Simanzi!
Mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu na Mwanzilishi wa Kanisa la Cathedral
of Joy (CoJ) na mwimbaji wa nyimbo za Injili, Askofu John Simon Komanya
aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa kisukari, yamekuwa gumzo baada ya
familia yake kufuatilia maziko kidijitali kwenye mtandao wa kijamii wa
Skype wakiwa Marekani.
Akizungumza na waandishi wetu, mchungaji msaidizi wa kanisa hilo, Abel Kigeli alisema Askofu Komanya alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu lakini Julai 29, mwaka huu hali yake ilibadilika na kukimbizwa katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar.
“Hali yake ilibadilika hivi karibuni na alipopelekwa Hindu Mandal hali ilizidi kuwa mbaya na Julai 4, akahamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na siku hiyohiyo Mungu alimpenda zaidi na kumpumzisha, lakini sisi kanisa tutaendeleza kazi yake kama alivyokuwa akiifanya enzi za uhai wake,” alisema Mchungaji Kigeli.
Waimbaji mbalimbali wa Injili walijumuika kwa pamoja kumzika Askofu Komanya ambapo waligawana majukumu mbalimbali na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa huku mwimbaji, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ akigeuka kivutio muda wa msosi kwa namna alivyokuwa akiwahudumia waombolezaji.
Kwa upande wake Akofu Mkuu wa Makanisa ya Calvary, Dunstan Maboya alisema: “Komanya alikuwa muimbaji kama waimbaji wengine lakini mimi nilipokutana naye kwa mara ya kwanza ndiyo nikamshauri akasomee uaskofu kwani waimbaji wengi huishia kuwa wachungaji tu.
Marehemu Komanya ameacha mke na watoto watatu, wawili wa kike. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amen.

Note: Only a member of this blog may post a comment.