Na Brighton Masalu
Mwigizaji Bongo, Esha Buheti,
licha ya kuwa ndani ya ndoa, amekiri kuchepuka na mcheza mpira mmoja
ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake.
Mwigizaji Bongo, Esha Buheti.
Akizungumza na Ijumaa, Esha aliweka wazi hisia zake kuwa kwa sasa ana
kifaa kipya chenye hadhi na amekuwa akitupia picha zake mitandaoni
kisha anazitoa.“Najua wambeya watataka kumchunguza mpenzi wangu wa sasa ndiyo maana namuweka mtandaoni kisha nafuta harakaharaka,” alisema Esha.
Esha alifunguka kuwa, pamoja na ‘kidumu’ alichonacho bado yuko kwenye ndoa yake na anamheshimu mumewe aliyezaa naye mtoto mmoja.

Note: Only a member of this blog may post a comment.