Dustan Shekidele, Morogoro
Inatisha! Ndani ya
Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, familia ya mwanaume aliyetambuliwa
kwa jina la Hamis Juma, imekumbwa na mauzauza baada ya kuamka ili kula
daku na kukutana na nyoka mwenye hirizi mlangoni.
Tukio hilo lililozua taharuki lilijiri
mapema wiki hii kwenye nyumba ya familia hiyo inayoishi Mtaa wa Mkota
Kata ya Kiwanja cha Ndege mjini hapa.
Baada ya kutonywa juu ya tukio hilo, Ijumaa lilifika kwenye familia hiyo alfajiri na kushuhudia nyoka huyo aliyekuwa na hirizi na kitambaa cheusi shingoni akiwa mlangoni.
“Wakati tukiwa sebuleni tunakula, tulianza kuona damu nzito ikisambaa kutokea mlangoni.
“Ilibidi tufunge mlango hadi alfajiri tuliamua kuwaita watu waje kushuhudia na kusaidia kumuondoa,” alisema Hamis.
Katika kutafuta msaada wa kumuondoa
nyoka huyo na kusafisha damu zilizozagaa, alitokea mjomba wa familia
hiyo ambaye jina halikupatikana akaanza kumtoa kwa kutumia mti, jambo
lililosababisha taharuki kwa watu waliokuwepo wakaanza kukimbia.
Baada ya kumtoa nyoka huyo, watu
walianza kumpiga wakitaka kumchoma moto lakini alitokea mwanaume
asiyefahamika akamkwapua na kuanza kukimbia naye mitaani.
Katika hali ya kushtua zaidi, nyoka huyo
alibadilika, akawa hana hirizi huku akionekana ‘kadogo’ jambo
lililoibua madai ya ushirikina hivyo watu wakamuua.
Baba mwenye nyumba hiyo, Hamis Juma.
Kwa upande wake mke wa Hamis, Mama
Nurdin ambaye ni mjumbe wa mtaa huo, alishtushwa na tukio hilo na kusema
familia yake imekumbwa na hofu kubwa.
Uongozi wa Kata ya Kiwanja cha Ndege
ukiongozwa na Diwani, Mohamed Matikula na Afisia Mtendaji, Diha Zongo
walifika eneo la tukio na kuwachukua baba na mama wa familia hiyo hadi
ofisi ya kata kwa mahojiano zaidi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.