Saturday, July 11, 2015

Anonymous

DAVIDO Athibitisha Ujio Wake Mpya na Mtukutu RIHANNA!

Muimbaji wa Nigeria, David Adeleke a.k.a Davido ameweka wazi kuwa msanii anayefata kufanya naye collabo ni bibie Rihanna.
davido rihanna
Staa huyo ambaye anawania vipengele vitatu kwenye tuzo za MTV MAMA , aliulizwa swali na shabiki kwenye mtandao wa Twitter, kuwa ni msanii gani mwingine wa kimataifa wa nje ya Afrika anayetarajia kufanya naye collabo? Na Davido akamjibu kuwa ni wengi lakini anayefata ni Rihanna.
davido tweets
Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi kama ni lini watafanya collabo hiyo na kama itakuwa kwenye album hii anayotarajia kutoa au ni mpango wa baadaye.
Katika album yake mpya anayotarajia kuitoa mwezi ujao, Davido amewashirikisha wasanii wakubwa wa kimataifa akiwemo, Trey Songz, Meek Mill na Akon.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.