Aliyekuwa mgombea udiwani wa Kata ya Chamwino Adrew Boniface akilia.
Dustan Shekidele, Morogoro
Adrew Boniface aliyekuwa mgombea udiwani
wa Kata ya Chamwino mkoani hapa kupitia Chadema na Mtangazaji wa Kituo
cha Radio Planet, amejikuta akitokwa na machozi baada ya kushindwa
kwenye uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.
…Akiwa mwenye masikitiko.
Tukio hilo lilitokea juzi wakati mgombea
huyo alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo hilo kufuatia hujuma
aliyofanyiwa na wakala wake kiasi cha kumfanya ashindwe katika dakika za
mwisho.
Akizungumza na wananchi wa kata hiyo
kwenye Viwanja vya Zahanati ya Chamwino huku machozi yakimbubujika,
Andrew alidai kuwa mmoja wa mawakala wake alihongwa ili kumhujumu,
kitendo ambacho kimemuumiza kwani anaamini alistahili kuibuka na ushindi
mnono.
“Awali sisi viongozi tulipita katika
vituo vyote na kujumlisha kura zilizobandikwa vituoni na kubaini
tumeshinda kwa kura nyingi na wananchi wakaanza kushangilia huku
wakishinikiza matokeo yatangazwe.“Hata hivyo, hayakutangazwa na baadaye
mmoja wa mawakala wetu alituambia kwamba wakala wetu katika zoezi hilo
la kuhesabu kura za jumla ametuhujumu na kukubali kwamba mgombea wa CCM
ndiye mshindi, jambo ambalo wananchi wangu wamelipinga,” alidai mgombea
huyo.
Kufuatia maelezo hayo, mgombea huyo
aliwapa hasira wafuasi wake walioanza kufanya vurugu kupinga ushindi wa
mgombea wa CCM, Benson Makanjira hali iliyosababisha polisi kuingilia
kati na kufanikiwa kuwatuliza.
Note: Only a member of this blog may post a comment.