Msanii wa muziki Nay Wa Mitego, Jumapili ya kesho (July 12)
anatarajia kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Sina Muda’, wimbo uliofata
baada ya ‘Mapenzi au Pesa’ aliyomshirikisha Diamond.
Nay ameleeza kwanini ameamua kutoa video ya wimbo mwingine kabla ya kutoa video ya ‘Mapenzi au Pesa’ iliyotangulia kutoka.
“Unajua Mapenzi au Pesa ilibidi iwe imeshaisha na iwe imeishatoka,” Nay Wa Mitego ameiambia Bongo5. “lakini
kama unavyojua hapo katikati Diamond alikuwa anapilika nyingi halafu
mimi mwenyewe pia nilikuwa sijatulia mambo yalikuwa mengi.”
Amesema kuwa wimbo wa ‘Sina Muda’ haukuwepo kwenye mipango ya kutoka
lakini mapokezi yake ndio yamemshawishi kuifanyia video, na kuongeza
kuwa video za Hip Hop ni rahisi zaidi kufanya.
“Uzuri wa hii imekuwa ni video moja nyepesi sana kama unavyojua
video za hip hop zinakuwaga ni simple sio complicated sana. Haikuwepo
kwenye ratiba nimeifanya tu fasta na nikaona ni wimbo tayari unatembea
kwa nguvu yaani wenyewe unatembea bila hata kusukumwa, nikaona ngoja
niupush kwa video lakini video ya Mapenzi au Pesa Jumatano tunashoot .”
Kuhusu kama haoni kuachia video mbili kunaweza kusababisha kuipunguzia nguvu ile atakayotangulia kuitoa hiki ndicho alisema Nay;
“Unajua hii ni miziki miwili tofauti, so sidhani kama inaweza
zikaathiriana lakini mwisho wa siku nafikiri zitapeana kama wiki mbili
tatu, mapenzi au pesa ikiisha nafikiri ndani ya wiki mbili baada ya
kuachia hii, so hii Jumapili inatoka ile itakuwa inayofata.”
‘Sina muda’ ambayo inatoka kesho imeongozwa na Director aitwaye Joowzey, na ‘Mapenzi Au Pesa’ itaongozwa na Hanscana.

Note: Only a member of this blog may post a comment.