Thursday, July 2, 2015

Anonymous

BREAKING NEWS: Bunge Laahirishwa Ghafla Baada Ya Wabunge wa UKAWA Kugomea Miswada!

#‎BUNGENI‬ Spika Makinda amelazimika kusitisha kikao cha bunge baada ya baadhi ya wabunge kusimama kupinga utaratibu wa uwasilishwaji miswada kwamba hautendi haki!

NEW UPDATES!
Kwa kile wanachokiita wanaburuzwa, Wabunge wa UKAWA kwa pamoja wamegoma kuendelea na bunge na wote kuamua kusimama baada ya kupinga uwasilishaji wa dharula wa Miswada mitatu muhimu ya Gesi, Petroli na Uziduaji "Extractive Industries".

Ni baada ya John Mnyika kuomba Muongozo juu ya uvunjaji wa kanuni za bunge. shuguli za leo zimekiuka kanuni kwani miswada imewekwa ikiwa sambamba. anasema hoja ikishatolewa ni lazima ijadiliwe iamuliwe ndo itolewe hoja nyingine, lakini leo zipo hoja tatu kwa pamoja.

Mnyika kasema na huu Muongozo sitaki useme utautolea ufafanuzi siku nyingine kwa maana hatuwezi kuendelea kufanya kazi ambazo zimevunja kanuni.

Wanapinga kuwasilishwa kwa dharula na kwa pamoja Miswada yenye manufaa makubwa kwa nchi.
Miswada wanayo pinga na iliyo wasilishwa kwa pamoja ni;

1.Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum Act, 2015):
2.Muswada juu ya Usimamizi wa Mafuta na Gesi, 2015 (The Oil and Gas Revenues Management Act, 2015):
3.Muswada juu ya tasnia ya Uziduaji Tanzania (The Tanzania Extractive Industries Act, 2015): The Tanzania Extractive Industries Act, 2015.

Hata baada ya Spika kuwataka watoke nje kama hawataki kuendelea, Wamegoma na kusimama na kuanza kupiga kelele hadi Spika akaahirisha bunge. UKAWA wamesema mwanaharamu hapiti leo.
Kusikiliza kilichoendelea bungeni leo live
Bonyeza HAPA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.