Chande Abdallah DIVA
wa filamu Bongo ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja anayetambulika
kwa jina la Cookie, Aunt Ezekiel, amefungukia kuhakikisha anampa sapoti
ya nguvu shosti wake, Wema Sepetu katika harakati zake za kuwania
ubunge.
“Kama rafiki wa Wema nitahakikisha nampa sapoti ya nguvu rafiki yangu hadi aingie mjengoni, japo kuwa mimi binafsi sipendi siasa na sitaki kujiingiza huko,” alisema Aunt Ezekiel.
Wema ni mmoja kati ya wasanii waliojitokeza katika kinyang’anyiro cha kutangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalumu jimbo la Singida Mjini kwa tiketi ya CCM.

Note: Only a member of this blog may post a comment.