Musa Mateja
WAKATI vioja vya kuelekea
uchaguzi mkuu vikiendelea huku wagombea wa nafasi mbalimbali wakikazana
kutangaza nia, mambo hayakuwa mazuri kwa Steven Mengere ‘Steve Nyerere’
alipokuwa akitangaza nia ya kugombea ubunge wa Kinondoni baada ya
mkutano wake kuvunjika kabla hajamaliza, Amani lina stori kamili.
Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita
katika Mtaa wa Bwawani, Kinondoni ambapo Steve Nyerere aliandaa mkutano
huo ambao awali aliuita wa kuhamasisha watu kujiandikisha katika daftari
wa wapiga kura.
Wakati Steve Nyerere akijinadi kuwa
anataka Kinondoni yenye mabadiliko katika kila sekta na kuhamasisha watu
wamchague, ghafla aliibuka Mwenyekiti wa Mtaa wa Bwawani, Omar Karembo
akamnyang’anya kipaza sauti na kusema:
Baada ya tamko hilo, vurugu za hapa na
pale ziliibuka ambapo watu walihoji kwa nini mwenyekiti huyo aliuvunja
mkutano pasipo kuanika sababu. Steve Nyerere alisaidiwa na baunsa kutoka
jukwaani akionesha dalili za kutaka kulia huku mwenyekiti huyo
akitokomea zake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.