Thursday, June 4, 2015

Anonymous

VIDEO+PICHAZ: Marekani imerudi tena kwenye Headlines za ubaguzi.. hii imetokea ndani ya ndege ikihusisha soda ya kopo !!

Neno ubaguzi ni kama lilianza kusahaulika hivi duniani.. lakini kwa sasa linasikika karibu kila siku, matukio ya watu wenye asili ya Afrika kupigwa risasi Marekani yalichukua headlines kubwa sana na bado hayajasahaulika !! 

Hiki kilichofanywa na mhudumu wa kwenye ndege ya Shirika la ndege la United Airlines, nacho kimelalamikiwa na kuhusishwa na ishu ya ubaguzi.. mhudumu huyo aligoma kumpatia abiria mmoja mwanamke, Tahera Ahmed soda ya kopo, alichomjibu ni kwamba eti hawezi kumpa kwa sababu anaweza kutumia kopo hilo la soda kama silaha ndani ya ndege.
Coke 
Mabosi wa Shirika hilo hawajaicha hii ishu hivihivi.. mhudumu huyo amesimamishwa kazi.
Kitu kilichomkasirisha zaidi Tahera ni ishu ya yeye kukataliwa soda ya kopo alafu jirani yake akapewa bia ya kopo.. mwanamke huyo akalalamika kwamba labda kwa vile yeye ana asili ya Kiarabu ndio maana akakataliwa !!
Hapa kuna video inayoonesha mwanamke huyo akielezea ilivyokuwa...Bonyeza play au download hapa chini...

Hii ilikuwa post ya Tahera kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya kutokea kwa ishu hiyo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.