Friday, June 5, 2015

Anonymous

BREAKING NEWS: AJALI MBAYA YAUA WANAFUNZI 7 WA KIDATO CHA NNE HUKO MBINGA, RUVUMA!

Habari kutoka mkoani Ruvuma zinasema kuwa wanafunzi 7 wa shule ya sekondari ya Misheni ya Kigonsela wilaya ya Mbinga wanadaiwa kupoteza maisha na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya katika gari linalomilikiwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la kijiji cha Kigonsela kata ya Kigonsela baada ya gari dogo aina ya Landrover 110
lenye milango mitano kushindwa kupanda mlima na kupinduka kwenye korongo kisha kuwaka moto.

Wanafunzi hao walikuwa wanatoka kwenye shamba la shule kurudi shule,walifuatwa na mkuu wa shule hiyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari Ngaiwona Nkondola aliyeongea na kamanda wa polisi mkoani humo,huenda ajali hiyo imetokana na kuzidiwa kwani ndani ya gari hilo kulikuwa na wanafunzi 16 pamoja na mwalimu wao huku juu ya gari (keria) wakiwa wamekaa wanafunzi zaidi ya 20 ambao wamejeruhiwa vibaya.
Taarifa kamili tutawaletea hivi punde........

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.