Thursday, May 28, 2015

Anonymous

Una Kipaji cha Kuigiza?! Kampuni Hii ya Eagles Inakuhitaji...


Yuster Nyakachara, mkurugenzi wa kampuni ya Eagles Entertainment
Kampuni ya Eagles Entertainment inayojishughulisha na utengenezaji wa muziki na filamu ipo katika mikakati ya kufanya usaili kwa ajili ya maandalizi ya kurekodi tamthilia kali na ya kipekee hapa Bongo, mkurugenzi wa kampuni hiyo Yuster Nyakachara anafafanua. 

Tutakuwa na zoezi la kutafuta wasanii wenye vipaji kwa ajili ya tamthilia yetu ambayo ni ya kipekee kabisa kutengenezwa na ratiba yetu ni kuanza kushuti mwezi wa saba,”anasema Mghesi.
Kampuni inatarajia kuanza kufanya usaili mapema hivi kwa mikoa ya Kilimanjaro, Kigoma, Arusha, na Dar es Salaam, kwa wale wote wenye vipaji ni wakati wao wa kujitokeza kuonyesha vipaji vyao baada ya matangazo kutoka na kukujulisha wapi usaili utafanyika.
Unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hii:- +255714 676 667 piga au tuma ujumbe tu siyo kubipu onyesha kipaji chako sasa!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.