Thursday, June 25, 2015

Anonymous

VIDEO: MSANII Rick Ross akamatwa kwa kosa la kuteka na kushambulia!

Rapper Rick Ross Jumatano hii alikamatwa na polisi huko Georgia kwa madai ya kumteka na kumshambulia mtu nyumbani kwake.
Mtu huyo anaidaiwa kushikiliwa na Ross kwa masaa kadhaa na kupigwa kiasi cha kujeruhi taya zake na hivyo kushindwa kutafuna chakula.

Ross, 39, ambaye jina lake halisi ni William Leonard Roberts, alishikiliwa na ‘the U.S. Marshals Southeast Regional Fugitive Task Force.’

Alishtakiwa kwa kosa linalohusiana na kushambulia kwenye kaunti ya Fayette anakotokea. Mlinzi wake Nadrian Lateef James naye amekamatwa kuhusiana na kesi hiyo.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa na mamlaka kuhusiana na kesi hiyo.
June 10, Ross pia alikamatwa akiwa na bangi kwenye gari lake.
Tazama video hiyo hapa chini... \

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.