Wednesday, August 5, 2015

Anonymous

SAD NEWS! MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA ST. JOSEPH SONGEA AFA KWA KUJINYONGA!

Na Gideon Mwakanosya, Songea
MWANAFUNZI wa mwaka wa pili wa chuo kikuu cha St. Joseph tawi la songea Mkoani Ruvuma Emmanuel Peter Lunguya (25) amekutwa chumbani kwake amekufa naada ya kujinyonga kwa kutumia kamba za viatu zilizokuwa zimefungwa kwenye kenchi la paa ndani ya chumba alichokuwa amepanga.
Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimezibitishwa na kamanda wapolisi wa Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela zimesema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa kumi ya jioni huko katika eneo la ruhuwiko karibu na shule ya msingi Manispaa ya Songea.

Kamanda Msikhela alifafanua kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Lunguya alikutwa chumbani kwake akiwa ananing’inia baada ya kujinyonga na majiranni walioshituka baada ya kuto onekana kwa siku mbili.

Alisema kuwa taarifa zaidi juu ya tukio hilo zinadai kuwa mara ya mwisho Lunguya alionekana chuoni kwake Julai 29 mwaka huu na siku ya alhamis ya wiki iliyopita alionekana akiwa hana tatizo lolote la kiafya licha ya kuwa kwa siku za nyuma aliwai kulazwa katika hospitali ya serikali ya mkoa Songea kwa muda wa wiki mbili na baadaye aliruhusiwa kurudi nyumbani.

Alisema kuwa Lunguya inadaiwa alilazwa katika hospitali hiyo baada ya kusumbuliwa na ugonywa wa akili ambao ndio uliokuwa unamsumbua kabda ya mahuti kumkuta.

Alieleza zaidi kuwa asikali polisi wa idala ya upelelezi walifanikiwa kufika kwenye eneo la tukio ambako marehemu alikuwa akiishina walifanya uchunguzi wa awali wakishilikiana na mganga wa hospitali ya serikali ya mkoa huo na kubaini kuwa Lunguya alijinyonga kwa zaidi ya siku tatu zilizopita kwani mwili wa marehemu huyo ulianza kuharibika.

Alisema kuwa Lunguya hakuna ujumbe wowote alio uwaacha kabdala ajachua uamuzi wa kujinyonga na pia hakuna mtu yeyote anayehusishwa na tukio hilo licha ya kuwa polisi inaendelea kufanya uchunguzi zaidi ya tukio hilo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.