Thursday, June 18, 2015

Anonymous

VAZI Hili Lapigwa Marufuku Kutokana na Tukio la UGAIDI Lililoua Watu 23 JuziI


Face Veils
Shambulio la Kigaidi limetokea Chad Jumatatu June 15 2015 katika Jiji la N’Djamena, watu 23 wakauawa na wengine zaidiya 100 wakapata majeraha makubwa. 

Waziri Mkuu wa Chad, Kalzeube Pahimi Deubet amesema mtu aliyelipua mabomu hayo alitumia vazi ambalo linavaliwa na wanawake wa kiislamu ambalo linaziba mpaka usoni… Kingine kilichoamliwa leo ni ishu ya kupigwa MARUFUKU kwa mtu yoyote kuvaa vazi hilo kwa mtu yoyote. 

Agizo lililotolewa leo June 18 2015 ni kwamba hakuna mtu yoyote anaeruhusiwa kuvaa vazi hilo popote ndani ya Chad… Japo haijathibitika ni nani kahusika na Shambulio hilo, stori mpaka sasa kutoka Chad zinataja sana kundi la Boko Haram kutokana na kitendo cha nchi hiyo kuisaidia Nigeria kupambana na Kundi hilo la wapiganaji.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.