Leo hii zimetoka taarifa nyingine ambazo zimeibua tetesi za siku
nyingi kwamba Raisi huyo wa FIFA alikuwa hana uhusiano mzuri na
mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo.
Gazeti lenye heshima kubwa nchini Spain – El Mundo limeripoti kwamba
aliyekuwa mchumba wa Ronaldo, Irina Shayk alikuwa na mahusiano ya
kimapenzi na Sepp Blatter katika vipindi viwili tofauti.
El Mundo linaripoti kwamba Blatter alikuwa na mahusiano ya muda mrefu
na Mrembo huyo wa kirusi, baada ya kuachana na mcheza tenis Ilona
Boguska lakini kabla ya kukutana na mwanamama Linda Barras, 50.
Habari hiyo ya Irina na Blatter imeandikwa kwenye na mwandishi wa gazeti la El Mundo Rosalia Sanchez
Anaelezea kwamba taarifa hiyo ya siri ya mahusiano ya Irina na Mzee
Blatter ilipata kutoka kwa chanzo chake cha kuaminika wakati anafanya
uchunguzi wa taarifa za rushwa na mahusiano zinamhusu boss huyo wa FIFA.
Uhusiano wao inasemekana ulianza mwaka 2002, wakatengana na kuja
kuendelea tena mwaka 2014, wakati Irina akiwa bado na mahusiano na
Cristiano Ronaldo ambaye walianza mwaka 2010 mpaka mwanzoni mwa mwaka
huu walipotangaza kuachana.
Taarifa ya mahusiano ya Blatter na Irina pia imeripotiwa katika
vyombo vya habari vya nchi za Peru, Portugal, Mexico na Vietnam pamoja
na kwenye mitandao ya kijamii..
Msemaji wa Irina Shayk alipoulizwa juu ya tuhuma hizi, hakujibu lolote. Hii ni kwa mujibu wa Dailymail ya Uingereza.

Note: Only a member of this blog may post a comment.