Na Saphyna Mlawa
UONGOZI wa Simba umesema muda wowote kuanzia sasa, unatarajia kutoa barua rasmi ya kumwagana na aliyekuwa kipa wao, Hussein Shariff ‘Casillas’.
Uongozi huo umefikia maamuzi hayo baada ya kuingia katika harakati za usajili kwa ajili ya msimu ujao ambapo wamesema kwa kuwa hawana ndoto za kuendelea na mchezaji huyo, wameona ni vema wakamfahamisha mapema ili afanye ustaarabu mwingine.
Casillas aliyekuwa kipa bora msimu wa 2013/2014, akiwa na kikosi cha Mtibwa Sugar, msimu ulioisha hivi karibuni mambo yalimuendea hovyo kutokana na kuuguza majeraha ya ugoko kwa muda mrefu, hivyo kuishia kusugua benchi, ingawa hali yake sasa imeimarika.
Ofisa habari wa timu hiyo, Haji Manara amesema ieleweke kuwa mchezaji huyo msimu ujao hawatamtumia ambapo muda wowote kuanzia hivi sasa wamepanga kumpa barua itakayomweka huru kutafuta timu nyingine kwa ajili ya kuitumikia msimu ujao.
“Hatuna ndoto za kuendelea na mchezaji huyo, ambapo kuanzia hivi sasa tunatarajia kumpa barua rasmi ya kuachana naye mapema kabisa ili naye afanye ustaarabu mwingine wa kutafuta timu ya kuitumikia msimu ujao.
“Msimu huu hakika Simba iko makini mno katika suala zima la usajili, malengo yetu ni kunasa saini zenye uhakika, japokuwa mambo yetu ya taratibu, lengo likiwa ni kufikia yale malengo tuliyojipangia,” alisema Manara.

Note: Only a member of this blog may post a comment.