Na Wilbert Molandi
KIUNGO mpya wa Yanga, Deus Kaseke na mshambuliaji wa timu hiyo, Malimu Busungu, wamezua tafrani kubwa kwenye kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars.
Tafrani hiyo ilizuka mara baada ya wachezaji hao kuondolewa kwenye kikosi cha Stars kilichoenda Zanzibar kujiandaa na mechi dhidi ya Uganda katika kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan).
Mara baada ya kuondolewa kwa wachezaji hao, chanzo cha habari kutoka ndani ya benchi la ufundi la Stars, kimeeleza kuwa kitendo hicho kimewakera baadhi ya viongozi kwenye Kamati ya Utendaji ya TFF.
Imeeleza kuwa viongozi walihoji sababu ya kuondolewa kwa wachezaji hao wakati uwezo wao ni mkubwa zaidi ya baadhi ambao bado wapo kikosini hapo.
“Kiwango kilichoonyeshwa na Kaseke kwenye mechi dhidi ya Rwanda ni ngumu kumuacha, pia kiwango cha Busungu alichokionyesha kwenye mechi hiyo na hata ligi kuu akiwa na Mgambo vinathibitisha ubora wao,” alilalama kiongozi mmoja wa juu. Wakati huohuo TFF imesema Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limemzuia Mrisho Ngassa haruhusiwi kucheza Chan kwa sababu siyo mchezaji wa ndani, hivyo Ngassa aliondolea kikosini kwa kuwa ameshasaini mkataba wa kujiunga na Free State Stars ya Afrika Kusini.

Note: Only a member of this blog may post a comment.