Friday, June 19, 2015

Anonymous

Mzungu mpya SIMBA SC atoa masharti mazito!

Khadija Mngwai na Mohamed Mdose
UONGOZI wa Klabu ya Simba, umepanga kufanya mabadiliko makubwa katika benchi la ufundi, ikiwa ni moja ya sharti la kocha mpya atakayetua klabuni hapo ambapo inaelezwa ni raia wa Uingereza.

Simba iliachana na Goran Kopunovic baada ya kutoafikiana katika suala la maslahi ya mkataba mpya, hivyo inaelezwa kuwa ipo katika hatua za mwisho kumleta Muingereza huyo ambaye atatua mwezi ujao.

Kikizungumza na Championi Ijumaa, chanzo cha kuaminika kutoka Simba kimeeleza kuwa, kocha huyo ambaye jina lake limekuwa likifichwa na viongozi wa klabu hiyo, ametoa sharti la kutua kikosini hapo na memba wengine kwa ajili ya benchi la ufundi.

“Kocha tayari ameshapatikana, ndiyo huyo wa Uingereza unayemsikia lakini jina lake siwezi kuliweka wazi kwa sasa kwani hadi mipango itakapokaa sawa ndipo tutaweka wazi.

“Benchi lote la ufundi linatakiwa kubadilishwa kuanzia kocha msaidizi hadi kocha wa makipa wote wanakuja wapya hivyo hawa wa sasa wanatakiwa kuondoka. “Simba imejipanga kufanya mabadiliko ya nguvu katika kikosi chake kutokana na kuhitaji kufanya kweli msimu ujao ili kuweza kushiriki michuano ya kimataifa kutokana na kutoshiriki kwa miaka mitatu mfululizo,” kilisema chanzo hicho.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.