MSHTUKO! Mtoto
mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amezua gumzo ukumbini baada
ya kuonekana akiwa amevaa pete iliyoaminika kuwa ni ya uchumba na
kusababisha minong’ono miongoni mwa mashabiki wake.
Mpango mzima ulijiri wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Sinema wa
Mlimani City (Cinemax) kulipokuwa na uzinduzi wa sinema ya 10 Bora ya
washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talent, mwaka jana ijulikanayo
kama Mpango Mbaya.
Punde tu baada ya Lulu kuwasili ukumbini hapo mishale ya saa mbili
usiku akiwa na mashosti zake, minong’ono iliibukia kwenye zulia jekundu
wakati mrembo huyo alipokuwa akifotolewa picha na mapaparazi ndipo
wapenda ubuyu walipoanza kusambaziana habari hali iliyosababisha watu
wengi kutaka kumuona Lulu.
“Ile
ni ya uchumba aise atakuwa amechumbiwa, afadhali Lulu achumbiwe na
aolewe sasa japo bado anasoma lakini kwa kuwa ni chuo ni vyema na haki
akaendelea na uchumba wake huku akimalizia masomo na kisha ndoa
ikafuata,” alisikika mmoja wa mashabiki akiwaambia marafiki zake.
Baada ya watu kuanza kumzingira eneo hilo kutaka kuishuhudia pete
hiyo, haraka sana Lulu aliondoka eneo hilo na kwenda kujibanza ukumbini
kufuatilia sinema hiyo iliyokuwa imeshaanza kuoneshwa.
Paparazi wetu alifanya jitihada za kuzungumza na Lulu ili aweze
kumsikia anazungumziaje pete hiyo iliyopamba kidole chake lakini
hakutaka kuzungumzia lolote akidai hayupo tayari kufunguka lolote
ukumbini hapo.
Hata baada ya muvi kuisha, paparazi wetu aliendelea kumfuatilia Lulu
wakati anatoka ukumbini lakini pia hakutoa ushirikiano ambapo alionekana
kukataa kupigwa picha pamoja na kujibu maswali ya waandishi wa habari.

Note: Only a member of this blog may post a comment.