Imelda Mtema
STAA wa filamu za
Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ ameonekana kuchezea ‘sharubu’ za Kajala
baada kuweka picha ya kiazi kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram
kitu ambacho kimeonekana ni kumkejeli staa mwenzake huyo kutokana na
Wema Sepetu kumuita kiazi.
Kwa upande wa Kajala alipoulizwa kama kuna tatizo lolote kati yake na Batuli alifunguka;
“Sijui kama mtu ana bifu na mimi basi ni yeye tu na kama mtu anaposti kitu kwa ajili ya kuniumiza naona ni kazi bure tu kwa kuwa vitu hivyo vinapita na maisha yanaendelea siku zote.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.