KUFUATIA KUVAA NUSU UCHI! FAIZA WA MH. SUGU AOMBA MSAMAHA KWA WATANZANIA!
Mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Faiza Ally.
Imelda Mtema MZAZI mwenzake na
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Faiza Ally, hivi karibuni
katika tuzo za KTMA aliwaacha watu midomo wazi baada ya kutinga na
kivazi kilichoacha sehemu kubwa ya makalio yake nje na kuzua minong’ono
katika mitandao ya kijamii.
Akizungumza
na Amani kwa kuonekana kujutia kitendo kilichotokea, Faiza alisema kuwa
ile nguo aliishona ikiwa imeziba sehemu yote ya nyuma japokuwa ilikuwa
imechanwachanwa lakini hakuwa na nia ya kuacha sehemu ya makalio yake
nje.
Akiendelea kuzungumza alisema kuwa, siku alipokuwa akienda kwenye
tuzo alikuwa peke yake kwenye gari hivyo alivyoinuka ndiyo ile nguo
ikapanda bila kufahamu.“Jamani siwezi hata siku moja kujiachia hivyo
naomba Watanzania wanisamehe,” alisema.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.