Said Ally na Nassor Gallu
KIUNGO wa timu ya Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho pamoja na mshambuliaji mpya, Malimi Busungu ni kama pacha yao imeonekana kuelewana katika kikosi hicho kutokana na kucheza kwa viwango vya hali ya juu huku Coutinho akimtengenezea Busungu pasi mbili za kufunga.
Katika mazoezi ya jana ya Yanga ambayo leo inashuka dimbani kumenyana na timu ya Friends Rangers kwenye mchezo wa kirafiki utakaopigwa Uwanja wa Karume, Coutinho na Busungu walionekana kuelewana vilivyo, hali iliyowafanya mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza kushuhudia mazoezi hayo kuwashangilia kila mara.
Hata walipotenganishwa vikosi viwili, wachezaji hao walikuwa wanaendeleza makali yao huku wakiibua minong’ono kwa mashabiki.
KIUNGO wa timu ya Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho pamoja na mshambuliaji mpya, Malimi Busungu ni kama pacha yao imeonekana kuelewana katika kikosi hicho kutokana na kucheza kwa viwango vya hali ya juu huku Coutinho akimtengenezea Busungu pasi mbili za kufunga.
Katika mazoezi ya jana ya Yanga ambayo leo inashuka dimbani kumenyana na timu ya Friends Rangers kwenye mchezo wa kirafiki utakaopigwa Uwanja wa Karume, Coutinho na Busungu walionekana kuelewana vilivyo, hali iliyowafanya mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza kushuhudia mazoezi hayo kuwashangilia kila mara.
Kiungo mpya wa Yanga, Malimi Busungu.
Championi Jumatano lililokuwepo uwanjani hapo,
lilishuhudia wachezaji hao wakifanya mavitu hayo wakati kocha wao, Hans
van Der Pluijm alipowapa zoezi la kupiga krosi na kufunga ambapo Busungu
alionekana kuzitumia vyema krosi za Coutinho na kufunga mabao mawili
safi kwa kichwa.Hata walipotenganishwa vikosi viwili, wachezaji hao walikuwa wanaendeleza makali yao huku wakiibua minong’ono kwa mashabiki.

Note: Only a member of this blog may post a comment.