Saturday, June 6, 2015

Anonymous

NISHA WA BONGO MUVI AWASHTAKIA WEZI KWA MUNGU!

Gladness mallya
Baada ya wezi kumfanyia kitu mbaya kwa kumuibia vifaa kibao kwenye gari lake na kuliacha kama gofu, staa wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameamua kufunga siku saba kwa ajili ya kuwashtaki wezi hao kwa Mwenyezi Mungu.

Staa wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Akizungumza na paparazzi wetu, Nisha alisema kwa siku hizo saba ataomba dua maalum na hatatoka nyumbani kwenda sehemu yoyote na hii ni kwa ajili ya kuwashtakia kwa Mungu wale waliomuibia vifaa vya gari na fedha kwani anajua dua ndiyo kila kitu. 

“Niko kwenye mfungo wa siku saba kwa ajili ya kuwashtaki wale walioniibia maana najua Mungu ndiye aliyenipa na hao walioniibia atawalipa sawasawa na ubaya wao, sijafanikiwa kumjua hata mmoja lakini najua Mungu anawajua na atawalipa kwa wakati wake,” alisema Nisha.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.