JACOB Steven Mbura ‘JB’ anaendelea kusimulia historia ya maisha yake tangu utotoni hadi sasa. Ni simulizi ndefu na tamu isiyochosha kwa vimbwanga na kila aina ya mikasa ya kusisimua na kustaajabisha. Uhondo huu ulianza wiki mbili zilizopita. Kwa wale waliokosa kwa bahati mbaya, tuliweka nukta kwenye kipengele cha safari yake ya shuleni na malezi ya nyumbani, ambapo alieleza hatua kwa hatua. Je, nini kinaendelea? Teremsha macho hapa chini, twende mdogomdogo.
WAKATI JB akijiandaa kuendelea na simulizi, ghafla tukasikia vishindo vya hatua za mtu akielekea mahali tulipokuwa tumekaa. Sote tukasitisha kidogo mazungumzo na kwa pamoja tukageuka kutazama kujua ni nani. Ni hapo ndipo nilipomuona JB akitabasamu! Alikuwa ni yule mhudumu aliyemuagiza chakula wakati tunaanza mazungumzo.
“Nikuambie kitu Brighton?,” aliniuliza huku akishika kiti chake kwa mkono mmoja na kukisogeza karibu kabisa na meza.
“Mmmh,” niliitikia kwa kuguna na kisha kumkazia macho kidogo nikiwa nimesitisha kuandika chochote!
“Hili ndilo eneo ambalo huwa natulia kabisa, msosi? Weee, ufundi wote huwa naumalizia hapa, acha tule kwanza ndipo hayo mengine yafuate,” alisema mfululizo huku akitumbukiza mikono yake kwenye chombo cha kunawia huku akimkagua kwa macho mhudumu huyo kwa kumwangalia kutoka juu hadi chini.
Baada ya kumaliza zoezi la kula, JB akaendelea na simulizi.
“Enhe…, ikawaje baada ya hapo?,” nikamtupia swali wakati namalizia kujifuta maji mkononi.
“Mwaka 1992, nilijiunga na chuo cha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hukohuko Tanga, eneo moja linaitwa Kabuku, kwa kipindi cha mwaka mmoja kama ilivyokuwa ikihitaji sheria ya wakati huo,” anasema JB.
Hapohapo, nikataka kujua kwa kina zaidi maisha yake jeshini yalikuwaje?
“Kama unavyojua maisha ya jeshi hayana lelemama, hivyo yalikuwa ya sulubu sana kwa upande wangu hususan siku za mwanzoni, lakini baadaye mambo yakakaa sawa,” anasema JB.
Ghafla mazungumzo yetu yanakatishwa na mhudumu akidai pesa yake ya chakula. Haraka sana namuona JB akilala ubavu na kuchomoa waleti yake ambayo kamwe huwezi kuitazama mara moja tu. Anachomoa noti mbili nyekundu (20,000/=) na kumpa mhudumu aliyekuwa amejiandaa kumrudishia chenji na JB kumtaka abaki nayo yote, ikiwa kama usafiri.
“Nashukuru sana kaka, Mungu akubariki sana,” alisema yule mhudumu huku akiondoka kwa kutazama nyuma mara kwa mara hadi alipopotea kwenye upeo wa macho yetu.
“Basi bwana, na hapa nataka niweke wazi jambo moja muhimu kuwa, maisha ya jeshini yalinitia adabu sana,” anasema JB huku akiegemea kiti chake na kurekebisha mkanda wa suruali kwa kuchomekea vyema.
Kufika hapo, najikuta napiga picha ubongoni mwangu kama namuona jinsi alivyokuwa akisulubika jeshini. Napata shauku zaidi ya kumsikiliza nguli huyu wa sanaa ya uigizaji kwa sasa.
“Kwa mara ya kwanza maishani mwangu kushika jembe na kulima ilikuwa jeshini, asikuambie mtu mdogo wangu, ilikuwa ni balaa,” anasema na kuachia kicheko kwa sauti ya juu. “Kwa hiyo nilisota sana kwa siku za mwanzo, baadaye nikazoea na maisha yakasonga kambini hapo,” anasema JB kwa sauti ya chini sana iliyojaa upole na kumbukumbu nyingi! “Dah!, ikawaje kaka?,” nikamuuliza nikiwa na hamu kubwa ya kujua maisha yalivyokuwa hapo chuoni.
“Kama nilivyosema hapo awali, maisha yaliendelea baada ya kuzoea sulubu za kijeshi,” anabainisha na kabla hajaendelea, ghafla namuona aki..

Note: Only a member of this blog may post a comment.