Imelda Mtema
Muuza nyago kwenye video za wasanii
wa Bongo Flava, Tunda Sabasita amejitapa kumpora bwana muuza nyago
mwenzie, Agness Gerald ‘Masogange’ na kusababisha wawili hao kuingia
kwenye bifu zito.Sosi aliye karibu na wauza nyago hao alisema kuwa bifu
walilonalo linamhusu bwana aliyetajwa kwa jina moja la Said ambaye
makazi yake ni nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’.
Baada ya habari hiyo kutua kwenye Dawati la Ijumaa, mwandishi wetu alimsaka Masogange ambaye alikuwa mkali na kusema kuwa yeye hamfahamu Tunda wala hapendi kusikia habari hizo.
“Kwanza simjui huyo Tunda wala sitaki kujua habari zake hata kidogo, naomba mniache,” alisema Masogange.
Tunda aliposomewa mashtaka yake alikiri kugombana na Masogange na kusema mwanaume huyo alipomfuata alimwambia walishaachana na Masogange hivyo yeye hana kosa.
“Said aliniambia wala sikujua kama alikuwa na Masogange, alisema walishaachana hivyo atulize presha hakuna sababu ya kuwapa watu faida,” alisema Tunda.

Note: Only a member of this blog may post a comment.