Gladness Mallya na Hamida Hassan BAADA
ya kukataa sana, hatimaye mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’ amenaswa
nyumbani kwa mwigizaji Ester Kiama ambaye inadaiwa kuwa ni mpenzi wake.
Makachero wetu walifika mapema eneo la tukio na kujibanza sehemu ambapo ulipofika muda muafaka, Dude aliingia katika geti la nyumba hiyo ya Ester akiwa na gari aina ya Toyota Mark II kisha Ester akatoka kumpokea.
Wakizungumza jambo.
Walipokuwa wanaingia ndani, Dude aliwashtukia mapaparazi wetu
waliokuwa bize kuwafotoa ‘mapicha’ ndipo aligeuka mbogo kwa kurusha
matusi na kukataa kutoa ushirikiano kwa waandishi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.