Chande Abdallah na Deogratius Mongela
INATISHA!
Familia ya Zidadu Kasimu (34) inayoishi Mlandizi, Pwani inakumbwa na
mauzauza nyakati za usiku kwenye nyumba yao baada ya wageni wanaofika na
kulala vyumbani kusimulia visa vya kutisha vinavyohusisha ushirikina.
“Yaani kaka ilifikia hatua wageni wakija wanakimbia usiku, wengine wakiamka wanaondoka bila kuaga na hawarudi tena, sasa tumefunga vyumba hivyo tunalala wote chumba kimoja ambacho hakina mauzauza,” alisema Zidadu.
Mke wa Zidadu, mama Mau alisema licha ya mauzauza, pia kuna wakati fedha zao hupotea kiajabu na kuna siku walishangaa kuona mfupa ukitoka chooni na kuingia uvunguni mwa kitanda jambo lililowashtua sana.

Note: Only a member of this blog may post a comment.