Friday, June 5, 2015

Anonymous

HAKUNA MSANII ASIYEPENDA KUFIKA ALIPOFIKA DIAMOND -CHRISTIAN BELLA Afunguka!

Mwanamuziki Christian Bella
Christian Bella anaamini kuwa kikwazo cha wasanii wengi kukua kutokuwa na management. Bella ameiambia Bongo5 kuwa kila msanii ana lengo la kwenda mbali zaidi lakini tatizo lipo kwenye management.

“Muziki wetu bado una matatizo mengi ndo maana unaona kuna wakati unahitaji kufanya kitu lakini unashindwa. Hakuna msanii asiyependa kufika alipofika Diamond, kila mtu anataka, tatizo ni management,” amesema msanii huyo.

“Kila msanii huwezi kutumia pesa yako ya mfukoni kutengeneza video, hautaweza kufika popote. Management ndIo inaweza kukusimaMia kila kitu, lakini sisi hapa kila kitu anafanya msanii huyo huyo, hatuwezi.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.