Monday, May 18, 2015

Anonymous

ZA MWIZI 40: BINTI ALIYETUHUMIWA KUIBA MTOTO HUKO MOROGORO ANASWA!

Dustan Shekidele, Moro
SIKU chache baada ya gazeti hili kuripoti kuibiwa kwa mtoto lrene Daniel mwenye umri wa siku 34, mkazi wa Kilakala, mkoani hapa, habari njema ni kwamba mwizi wa mtoto huyo amenaswa laivu, Ijumaa Wikienda lina full stori.
Huyu ndio mama aliyeibiwa mtoto wake Mei 8 mwaka huu huko mkoani Morogoro.
Mtoto huyo aliibiwa kimafia Mei 8, mwaka huu wakati mama yake Martha Masawe akiwa kwenye foleni katika Kliniki ya Nunge mkoani hapa. 

Baada ya habari hiyo kuchapishwa Mei 10, mwaka huu, wananchi wa Kitongoji cha Mikumi Wilaya ya Kilosa mkoani hapa walimtilia shaka mkazi mwenzao Jesca Patrick (23) ambaye ghafla alionekana akiwa na mtoto mchanga mara baada ya kutoka Morogoro mjini wakati hawakuwahi kumuona akiwa na ujauzito.
Huyu ndo mama anaedaiwa kuiba mtoto ambaye alifahamika kwa jina la jesca.
“Waliposoma habari ya kuibiwa mtoto gazetini halafu ghafla wakaona Jesca ana mtoto mchanga, wakamtilia shaka na kutoa taarifa polisi katika Kituo cha Polisi cha Mikumi, akakamatwa,” kisema chanzo chetu.
Mama aliyeibiwa mtoto akiwa na aliyedaiwa kuwa mwizi wa mtoto wake.
Mwanahabari wetu alifika kituoni hapo na kumshuhudia Jesca akiwa chini ya ulinzi wa polisi ambapo alipoulizwa kama ni kweli alimuiba mtoto huyo, alikiri kutenda kosa hilo na kuomba asamehewe. 

”Siwezi kubisha ni kweli nilifanya jaribio la kumuiba mtoto huyo kwani nilifanya juhudi za kuzaa lakini bahati mbaya mpaka leo sijabahatika kupata mtoto hivyo naomba mnisamehe,” alisema Jesca ambaye ni mkazi wa Mikumi. 

Kwa upande wake Martha, alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa kweli nalishukuru sana gazeti hili, yaani nilitamani nife kwa kumkosa mwanangu. Pia nalishukuru jeshi la polisi kwa kufanikisha kumpata mtoto wangu akiwa hai na afya njema na kumtia mbaroni mtu aliyemuiba,nimefurahi sana,” alisema Martha.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.