Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi jana uligeuka shubiri kwa Waziri Samuel Sitta wakati alipobanwa na wabunge kutokana na Serikali kushindwa kuboresha usafiri wa reli na anga.
Wabunge hao, mbali na kuibua ufisadi mbalimbali unaofanywa na watendaji wa Serikali, wakiwamo wa wizara hiyo, walihoji sababu za Serikali kuwa na ndege moja tu na kushindwa na nchi ndogo ya Rwanda ambayo ina ndege saba za serikali.
Licha ya kuipitisha, walisema kuwa nchi bila kuwa na usafiri unaoeleweka wa reli, anga na barabara ni vigumu kupata maendeleo.
Akichangia mjadala huo, mbunge wa Kawe, (Chadema), Halima Mdee aliibua suala la ukiukwaji wa mauzo ya nyumba za Shirika la Reli Tanzania na Zambia (Tazara), kwamba mbali na ukiukwaji wa mauziano na ununuzi, pia mfanyabiashara aliyenunua nyumba hizo amekwepa kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia Sh4 bilioni
“Haiwezekani, tuna taarifa hizo, nyumba zimeuzwa kwa bei ya soko na Serikali pia ilipaswa kupata kodi yake inayofikia wastani wa Sh4 bilioni… Serikali hii ni ya aina gani ambayo kila mwaka kuna kashfa za ufisadi katika wizara zake,” alisema Mdee.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, alisema katika serikali ya Awamu ya Nne kila wizara inakabiliwa na wizi, akifafanua jinsi Mamlaka ya Manunuzi Nchini (PPRA) ilivyoshindwa kufuata vigezo ya ununuzi wa mabehewa 124 ya Kampuni ya Reli (TRL).
Alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na utangazaji wa zabuni kutozingatiwa na pia kutofanyika kwa uchunguzi.
Alisema waziri wa uchukuzi na katibu mkuu wa wizara hiyo na waziri wa fedha ambao ndio waidhinishaji wa fedha hizo za ununuzi wa mabehewa wanatakiwa kuwajibika. Alisema suala hilo linalohusu Sh230 bilioni haliwezi kufunikwa na kupita.
“Kampuni feki ya kijanjanja, kati ya Sh166 bilioni zilizoahidiwa na wafadhili walitoa Sh6 bilioni tu. Sakata la Escrow limefanya msiaminike tena na hivyo kuwafanya wafadhili watoe asilimia nne tu ya fedha zote,” alisema.
“Wananchi chagueni Ukawa ili kurejesha heshima ya nchi na kuiondoa Serikali hii ambayo kwa ‘mission town’ haitarejesha heshima ya nchi kimataifa.”
Alisema Rwanda ni nchi ndogo lakini ina ndege saba wakati Tanzania ni nchi kubwa lakini ina ndege mmoja tena inahitaji matengenezo kila siku.
Mbunge wa Kisarawe (CCM) Suleiman Jaffo alisema watendaji wamekuwa wakihujumu nchi ili kuiharibia serikali ya CCM.

Note: Only a member of this blog may post a comment.