Gari iliyombeba Mbunge wa Jimbo
la Monduli, Mh. Edward Lowassa ikipita nje ya uwanja wa Sheih Amri
Abeid, jijini Arusha mapema leo asubuhi wakati akielekea kwenye ofisi za
CCM mkoa wa Arusha.
Lowassa akisaini kitabu cha
wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM mkoa wa Arusha. Kushoto ni
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole.
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa
Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache mbele ya Mtangaza
nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa alieambatana na
Mkewe, Mama Regina Lowassa pamoja na wanaCCM wengine.
Note: Only a member of this blog may post a comment.