Saturday, May 30, 2015

Anonymous

WIZ KHALIFA: SEBA AKINIIGA TATOO, ITANIUMA!

Zilipendwa wa Mwanamitindo Amber Rose, Wiz Khalifa.
New York, Marekani ZILIPENDWA wa Mwanamitindo Amber Rose, Wiz Khalifa ameeleza kuwa anampenda sana mwanaye Sebastian ila ataumia sana kama ataiga tabia zake ikiwemo ya kujichora tatoo.
Wiz Khalifa akiwa na mwanaye Sebastian.
Akizungumza na Jarida la People hivi karibuni, Wiz alisema kuwa, kinachomfanya ampende ni uzuri wake na jinsi anavyoonekana kuja kuwa mtu wa aina flani katika jamii.
“Nampenda sana Seba, ila kuna mambo akiniiga nitaumia sana. Moja ni hili la kujichora tatoo, akikua kisha akafanya hivyo, nitaumia sana kwani atakuwa ameiharibu ngozi yake nzuri,” alisema Wiz. Mwanamuziki huyo ana tatoo zipatazo 18 mwilini,zote zikiwa ni kwa ajili ya kuwapa heshima watu muhimu katika maisha yake.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.