Stephen Wassira akitangaza nia ya kuwania Urais kwenye Ukumbi wa wa BOT jijini Mwanza leo.
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira leo ametangaza
nia ya kuwania Urais kwenye Ukumbi wa wa BOT jijini Mwanza.
Wassira anawania nafasi ya kugombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katika hotuba yake wakati wa kutangaza nia yake, Wassira amesema
amepata kuteuliwa kuongoza sehemu mbalimbali nchini maana marais wote wa
awamu nne walikuwa na imani naye.
Pia amewashukuru wageni waalikwa waliofika kwenye ukumbi kutoka
sehemu mbalimbali kwa kuweza kufika na kumuunga mkono huku wakiwa na
imani naye.
Kauli mbiu yake ni katika mbio hizo ni Uchumi Imara kwa Tanzania mpya.

Note: Only a member of this blog may post a comment.