WEMA SEPETU, PENNY WAJA NA HII...NI JIBU KWA ZARI NA DIAMOND PLATINUMZ!
Imelda Mtema STAA wa filamu
Bongo, Wema Sepetu na Mtangazaji Penniel Mwingila ‘Penny’ ambao wote
kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkali wa
Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ baada ya kuona habari za mwenza wao
huyo wa zamani akiwa na mpenziwe mpya, Zali zinapamba moto kila siku,
wameibuka na kudai hawababaishwi nazo, kwani hivi sasa wameamua kuingia
kazini kwa kufanya bonge la project.
Mtangazaji Penniel Mwingila ‘Penny’.
Akizungumza kwa niaba ya mwenzake, Penny alisema kelele za kila siku
wamezichoka na baada ya kukaa pamoja, wameona hiki ni kipindi cha kupiga
kazi badala ya kupoteza muda.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
“Tumeamua kuandaa filamu yetu ya pamoja ambayo ninaamini itakuwa ni
kali na ya aina yake. Tumepoteza muda mwingi na hivi sasa tunahitaji
kufanya kazi, tunachowaomba mashabiki wakae tayari kutupokea na hatutaki
tena kushabikia mambo ya Zari na Diamond kwa sababu hayatuhusu,”
alisema.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
on Wednesday, April 15, 2015
Note: Only a member of this blog may post a comment.