Mwanzoni mwa msimu wakati mholanzi Louis van Gaal alipokuwa na
matokeo mabaya – vyombo vya habari vilikuwa vikitoa takwimu mara kwa
mara na kumfananisha na kocha aliyefukuzwa Man United – David Moyes.
Safari hii zimetolewa takwimu za makocha hao katika kuiongoza Man United
katika mechi dhidi ya timu kubwa sita za juu.
LVG amemuacha mbali Moyes – akiwa na ameshinda asilimia 62.5% ya mechi dhidi ya vilabu vya Top 6 huku David Moyes akiwa na rekodi mbaya ya kushinda 8.33% tu ya mechi hizo.
LVG amemuacha mbali Moyes – akiwa na ameshinda asilimia 62.5% ya mechi dhidi ya vilabu vya Top 6 huku David Moyes akiwa na rekodi mbaya ya kushinda 8.33% tu ya mechi hizo.
Manchester United walipata taabu mwanzoni mwa msimu lakini hivi
karibuni wamekuwa kwenye kiwango kizuri wakizifunga timu Tottenham,
Liverpool, Aston Villa na jana wakaipa kipigo cha mbwa mwizi Man City.
David Moyes aliweza kushinda mechi moja tu kati ya 12 alizoiongoza United dhidi ya Vilabu 6 bora kwenye ligi na United wakamaliza ligi wakiwa nafasi ya 7.
David Moyes aliweza kushinda mechi moja tu kati ya 12 alizoiongoza United dhidi ya Vilabu 6 bora kwenye ligi na United wakamaliza ligi wakiwa nafasi ya 7.
United sasa wanashika nafasi ya 3, wakiwa wanaongoza kwa kupata
matokeo mazuri dhidi ya timu zote za Top 6 – huku wakiwa wamebakiwa na
mechi 2 tu za vilabu vya juu – Chelsea na Arsenal – lakini Van Gaal
ameshaiongoza United kushinda mechi 5 kati ya 8 alizocheza.

Note: Only a member of this blog may post a comment.