Sunday, April 19, 2015

Anonymous

Soma Maneno Haya Ya Busara Toka Kwa WASTARA!

Staa wa Bongo Movies, Wastara Juma amesema kuwa anajitahidi kugawa muda wa kuigiza na biashara ili kwenda na kasi ya maisha inayohitaji uwekezaji zaidi 

Alisema akili inatakiwa ifikirie kitu zaidi ya kimoja cha kuingiza kipato na kujiaandaa na maisha yajayo badala ya kutegemea kazi moja . Alifafanua kwamba kipaji hakizeeki, lakini itafika wakati kama binadamu umri utakwenda na utahitaji kupumzika na kuacha mikiki mikik ya filamu, hivyo kama haukujipanga mapema itakuja kuwa shida. 

Alisema maisha yanahitaji maandalizi kipindi bado ana nguvu hivyo ameamua kuingia kwenye biashara ya mmavazi, mikoba na viatu ilikujiwekea akiba ya kufanyia mambo ya msingi siku zijazo. 
“Nina watoto wanaohitaji kusoma, mimi ndiyo baba, mama, lakini mimi mwenyewe nimejipanga kwa ajili ya siku zijazo, siyo biashara tu nahitaji kufanya vitu vingi vya kuniingizia kipato mabli na uigizaji”, alisema Wastara.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.