Tuesday, April 21, 2015

Anonymous

PICHAZ: DAMU YAMWAGIKA MOSHI! MAJAMBAZI WAUA WAWILI NA KUPORA PESA ZA KAMPUNI YA BONITE

Dereva wa Kampuni ya Bonite aliyetambulika kwa jina moja la Mselemu mara baada ya kushambuliwa kwa risasi na majambazi.
Mlinzi wa Kampuni ya Bonite, aliyetambulika kwa jina la Shamba baada ya kupigwa risasi na majambazi mjini Moshi.

...wakiwa kwenye gari baada ya kushambuliwa kwa risasi na majambazi.

Mlinzi baada ya kuuawa na majambazi.
MAJAMBAZI yaliyokuwa na silaha yamevamia gari mali ya Kampuni ya Bonite na kuwamiminia risasi dereva wa gari hilo aliyetambulika kwa jina moja la Mselemu na mlinzi wa Kampuni hiyo aliyetambulika kwa jina la Shamba kisha kupora fedha na kutokomea kusikojulikana. 

Tukio hilo limetokea jana mjini Moshi ambapo majambazi wanne waliokuwa kwenye pikipiki walivamia gari la Bonite lililokuwa likitoka kuchukua pesa za mauzo ya kampuni hiyo.
Taarifa zinadai kuwa dereva na mlinzi wa gari lililoshambuliwa walifariki palepale kutokana na kupigwa risasi nyingi sehemu mbalimbali za miili yao.

(PICHA NA GLOBAL WHATSAPP 0712 919 142)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.