Video mpya ya Ben Pol ‘Sophia’ iliyofanyika Dodoma na kutoka April
20,2015 imepokelewa vizuri na mashabiki wake na wengi wamemsifia kwa
uamuzi wa kumtumia msichana (video vixen) mwenye albinism.
Ben Pol amesema yeye na team yake walipanga kumtumia model mwenye albinism lakini haikuwa rahisi kumpata walipofika Dodoma, na huyo aliyeonekana kwenye video alisafirishwa kutoka Tabora kwaajili ya kazi hiyo.
“Huyu dada alitokea Tabora mimi sikuwa namjua kabla,” Ben Pol ameiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm. “Tulipokuwa pale Dodoma tukafanya kama msako hivi tukatembea kwenye vyuo vya Dodoma watu wanaokaa hostel tukawa tunapiga piga nao story huku sisi tukawa tunajua tunachotafuta lakini kwa pale Dodoma tukawa hatujafanikiwa halafu muda ukawa unaenda. Lakini kuna mmoja wetu kwenye crew akasema yeye ana ndugu yake yuko Tabora ndio akatuonesha picha nyingi nyingi tukaangalia tukajiridhisha[…]kwahiyo tukawasiliana na watu wa kwao familia nini mama wakakaa kikao wakamruhusu aje na ndugu yake mmoja.” Ben Pol ameongeza kuwa ameamua kumtumia model huyo ili kufikisha ujumbe kwa jamii kuwa watu wenye albinism wana haki ya kupendwa kama binadamu wengine.
-via bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.