Tuesday, April 21, 2015

Anonymous

MUNGU MKUBWA! BAADA YA KUZIMIA KWA MIEZI MIWILI, HATIMAYE BOBBI KRISTINA AZINDUKA!

Bobbi Kristina akiwa na baba'ke Bobby Brown.
Bobbi Kristina.
Bobbi Kristina ambaye ni mtoto wa nguli wa muziki Bobby Brown na marehemu Whitney Houston, amezinduka baada ya kupoteza fahamu kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na kilichoelezwa kuwa ni matumizi ya dawa za kulevya. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tovuti ya MTV na kuthibitishwa na Bobby Brown na shangazi yake, binti huyo amefumbua macho na sasa hatumii tena mashine ya kumsaidia kupumua. Binti huyo alikuwa mahututi kwa zaidi ya siku 75 na alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kukutwa ndani ya jakuzi nyumbani kwake januari 31, mwaka huu akiwa hajitambui. 
Kupitia ukurasa wa Facebook, Brown aliandika: “Kweli Mungu ni mkubwa, mpenzi wangu, binti yangu amefumbua macho na kunitazama. Ndiyo, hatumii mashine ya kupumulia tena, anapumua mwenyewe ingawa bado anapatiwa matibabu.
(Chanzo: MTV)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.